Hili ni toleo la pili la Kiswahili kwa Darasa la Nane. Kitabu hiki. cha wanafunzi ni cha nane katika mfululizo wa vitabu vinane vya lugha ya Kiswahili kwa shule za msingi. Kitabu hiki kimezingatia kwa kina na kwa namna ya kipekee mada zote zilizomo katika silabasi ya Kiswahili ya 2002 kwa Darasa la Nane. Katika toleo hili, masuala nyeti yameshughulikiwa kwa uketo na usasa kama vile utaratibu wa ngeli kwa kuzingatia upatanisho wa viambishi kisarufi. Masuala ibuka kama vile haki za watoto, mazingira, UKIMWI, uadilifu, jinsia, ajira za watoto na afya yameshughulikiwa kwa upana na utaalamu wa kupigiwa mfano. Mifano, michoro ya rangi na picha nyingi zimetumiwa ili kulifanya somo hili liwe la kuvutia zaidi. Mazoezi kemkem yanayozingatia vipengele vyote katika silabasi yamejumuishwa ili kumhusisha mwanafunzi kikamilifu. Kitabu hiki kinawalenga wanafunzi kutoka mazingira na jamii mbalimbali. Vilevile kitabu hiki kina mitihani ya majaribio ili kumwandaa mwanafunzi ipasavyo kwa mtihani wa K.C.P.E.
Reviews
There are no reviews yet.