Tamthilia ya Kigogo inamulika baadhi ya masuala yanayoibuka katika nchi zinazoendelea za Bara la Afrika. Huku wakazi wa Sagamoyo wakijiandaa kuadhimisha siku ya uhuru utakaosherehekewa kwa mwezi mmoja na kujivunia ‘maendeleo makuu’, Soko la Chapakazi, ambalo ndilo tegemeo la wengi jimboni, linafungwa ghafla. Je, viongozi wamelifunga kwa nia gani? Wakazi wa Sagamoyo wanaolitegemea kujipa riziki watafanya nini? Tamthilia hii inatoa picha halisi ya nchi inayojivunia miaka mingi ya uhuru. Je, uhuru huo unamfaidi nani?
Reviews
There are no reviews yet.